TUTUMIE MAONI AU HABARI KUPITIA EMAIL: clickhabari@gmail.com AU SIMU: +255 7557 758 909, : CCM MBELE KWA MBELE 2015

WAJUMBE WAANZA KUINGIA KWENYE UKUMBI WA MKUTANO HUKU MAJINA MATATU YAKIWA HADHARANI TAYARI


Kumekucha CCM Mchakamchaka 2015

Magufuli alivyopiga chenga panga la CCM

Dar es Salaam. Kama alivyowashangaza wengi pale alipojitokeza kuchukua fomu za kuomba kuteuliwa na CCM kuwania urais Mei 29 mwaka huu, ndivyo Dk John Magufuli alivyowashangaza tena jana kufikia hatua hii ya tano bora.
Bila makeke, majivuno wala majigambo, Magufuli ambaye ni waziri wa ujenzi alipochukua fomu alisema tu kuwa kipaumbelea chake ni kutekeleza ilani ya uchagzi ya CCM.
Hata katika safari yake ya kusaka wadhamini mikoani, mbunge huyo wa Chato alikwenda kimya kimya, bila mbwembwe, ahadi wala kukusanya mashabiki.
Bila shaka hiyo ndiyo siri yake ya ushindi, alihofia kukatwa mapema kwa kukiuka masharti ya chama, kama ilivyowatokea wengine.
Hata kabla hajachukua fomu, Dk Magufuli hakuwahi kutangaza nia yake ya kuwania urais, hadi alipoibuka ghafla na papo hapo akapenya hadi hatua hii muhimu, hadi alipolidokeza gazeti hili mjini Dodoma.


Edward Lowassa akatwa CCM

Dodoma. “Anakatwa, hakatwi” ndilo swali lililokuwa linaulizwa nchi nzima jana, lakini hatimaye Kamati Kuu ya CCM iliyokutana hadi usiku wa manane iliibuka na jibu kwamba Edward Lowassa amekatwa, huku kukiwa na wingu zito baada ya wajumbe watatu kupingana na uamuzi huo.

Kizungumkuti CCM, JK awataka wagombea wasinune.


Dodoma/Dar. Rais Jakaya Kikwete amesema idadi ya wanachama wa CCM waliojitokeza kuwania urais ni kubwa, hivyo ni lazima wawape viongozi muda wa kuwachuja lakini akawataka wasiwanunie baada ya kufanya uamuzi.
Rais Kikwete alisema hayo jana katika hotuba yake ya kuvunja Bunge ambayo iliibua waziwazi ushabiki kwa wagombea, hasa baada ya kumtaja aliyekuwa waziri mkuu wake wa kwanza, Edward Lowassa kwa ajili ya kumshukuru.

Mwisho Vichwa 33 leo

Dodoma. Kisu kikali cha Kamati Kuu ya CCM (CC) leo kitaondoka na vichwa 33 kati ya 38 vya walioomba kuteuliwa kupeperusha bendera ya chama hicho kumrithi Rais Jakaya Kikwete anayemaliza ngwe yake.
Kikao hicho ni hatua ya pili baada ya kukamilika kwa kikao cha Kamati ya Maadili kilichokutana jana usiku chini ya Mwenyekiti wa CCM, Rais Kikwete huku kikitawaliwa na usiri mkubwa, kuhama ukumbi na kila dalili za kubadili ratiba iliyopangwa awali ili kuvuruga mipango ya kambi za wagombea.



Kilichojadiliwa kwenye Kikao cha CCM Dodoma, Waziri Mkuu, Urais, Makundi..Maneno Ya Rais JK


Stori kuhusu Siasa zinapewa nafasi kubwa sana sasa hivi, Tanzania inaingia kwenyeUchaguzi Mkuu Mwezi October 2015… Tayari wapo waliotangaza Kugombea nafasi mbalimbali lakini macho ya wengi yako kwenye nafasi ya Urais, mpaka sasa kuna majina zaidi ya 35 ya watu waliotangaza Kugombea nafasi ya Urais kupitia CCM.
Rais Kikwete yuko Dodoma, imenifikia hii Ripoti ya kilichoendelea jana wakati wa Kikao cha Kamati ya Usalama na Maadili cha CCM.

Hii ni Tweet ya Rais JK aliyoweka muda mfupi uliopita

Mambo Yameanza Kupendeza Dodoma.......Tazama Picha 9 za Ukumbi Mpya Wa CCM Utakaotumika Kumtangaza Mgombea Atakayeteuliwa na CCM

Muonekano wa nje wa Jengo jipya la Ukumbi wa Mikutano wa kisasa wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoani....... Dodoma.
 
Ukumbi huu utaanza kutumika rasmi Julai 10 - 12, 2015 wakati wa Mkutano Mkuu wa CCM wa kupitisha jina la Mgombea Urais atakayeipeperusha bendera ya CCM kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwezi Oktoba mwaka huu. Ukumbi huu unauwezo wa kuchukua Watu zaidi ya 3000.



Dk Shein avuka hatua ya kwanza

Makamu wa Rais na Mjumbe wa Kamati Maalumu ya CCM Zanzibar, Dk.Mohammed Bilal (kushoto) akimpongeza Rais wa Zanzibar ,ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar , Dk Mohamed Ali Shein baada ya kuteuliwa kugombea nafasi ya urais kupitia chama hicho katika ukumbi wa ofisi za CCM Kisiwandui Zanzibar jana. Picha na OMR. Kabla ya wajumbe wa kamati maalumu kuanza kujadili ajenda ya mgombea wa nafasi ya urais wa Zanzibar katika kikao kilichofanyika Makao Makuu ya CCM Kisiwandui mjini Zanzibar jana, walimchagua kwa kauli moja Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Mohamed Gharib Bilal kuwa mwenyekiti wa kikao hicho.