Ndugu Wana-Arusha na Watanzania kwa Ujumla,
Napenda kutumia
fursa hii adhimu kuwatangazia kwa unyenyekevu mkubwa kwamba nitagombea
Ubunge Jimbo la Arusha Mjini mwaka huu wa 2015. Kipekee nitumie fursa
hii kumshukuru Mbunge anayemaliza muda wake (ndugu yangu, kamanda na
mjomba wangu, Mhe. Godbless Lema) kwa kuwaongezea watu wa Arusha hali ya
kuwa WAJASIRI; mimi nataka kuwapeleka mbele zaidi kwa kuwaonyesha na
kuwafungulia milango ya fursa za kimaendeleo ili tusiishie kuwa wajasiri
tu, bali sasa tuwe WAJASIRIAMALI na hivyo kujiletea maendeleo. Arusha
ni jimbo lenye watu makini sana, wanachohitaji kwa sasa ni kiongozi
mwenye maono, atakayewaonyesha njia sahihi ya kupita. Kiongozi huyo ni
mimi.
Natambua kwamba jimbo lina watu wa matabaka tofauti na
wenye itikadi tofauti na wakati mwingine zinazopingana sana, ila mimi
nakuja kuwa Kiongozi wa watu wote bila kuangalia tofauti zetu. Nakuja
kuwa baba, ambaye kwa kawaida, kama ana akili timamu na busara, huwalea
watoto wake wote kwa upendo bila kuwabagua kwa vigezo vyovyote vile; na
zaidi sana humkumbatia na kumbeba yule mtoto anayeonekana mnyonge, bila
kukata tamaa, ili na yeye siku moja afanikiwe. Nakuja kuwa Mbunge na
Baba wa Wana-CHADEMA na Wana-CCM (na vyama vingine vyote); Waislamu kwa
Wakristo (na dini nyingine zote); wasomi kwa wasiosoma; maskini kwa
matajiri; wanaosomesha watoto wao shule za kata (St. Kayumba) na
wanaosomesha International Schools; wanaotibiwa ndani ya nchi kwa
wanaotibiwa ughaibuni; wanaotembea kwenye barabara za lami na
wanaotembea kwenye barabara za vumbi na tope; wanaoishi uzunguni kwa
wanaoishi uswazi; wanaoishi kwenye nyumba za kupanga na waliokwisha
kujenga nyumba zao; wanaofanya shughuli zao kwenye sekta rasmi na isiyo
rasmi pia;
INAENDELEA.............
INAENDELEA.............