TUTUMIE MAONI AU HABARI KUPITIA EMAIL: clickhabari@gmail.com AU SIMU: +255 7557 758 909, : CCM MBELE KWA MBELE 2015

CCM ARUSHA YATOA ONYO KWA WALIOTANGAZA NIA ARUSHA MJINI.

 


 

Onyo hilo lilitolewa mwishoni mwa wiki iliyopita na katibu wa chama hicho wilayani Arusha,Ferooz Bano wakati akimkabidhi kanuni za uchaguzi wa CCM mgombea alliyetia nia ya kugombea jimbo la Arusha mjini kupitia chama hicho,Kim Fute .
Mgombea huyo alifika mbele ya ofisi za CCM wilayani hapa kujitambulisha  na kutia nia ambapo mbali na kufanyiwa ukaguzi wa kadi zake za uanachama pia alikabidhiwa kitabu chenye kanuni hizo na kupewa agizo la kutoshiriki kampeni kabla ya muda.
Hadi sasa jumla ya wagombea saba  ambao ni Kim Fute,Phillemon Mollel”Monaban”,Mustapha Panju”Bushbuck”,Victor Njau,David Rwenyagira,Deo Mtui,Francis Laiser pamoja na mbunge mstaafu wa jimbo la Arusha mjini,Felix Mrema wamejitokeza kutia nia kuwania jimbo la Arusha mjini.
Akizungumza mara baada kumkabidhi kanuni hizo katibu huyo wa wilaya aliwataka wagombea wote waliojitokeza kutia nia kupitia chama hicho kuacha tabia chafu ya kupakana kuandaa sherehe kwa wapiga kura.
“Muda wa kampeni bado haujafika hatutaki  nyinyi wagombea muanze kuchafuana huko mitaani na wala kuandaa vijisherehe”alisema Bano
Hatahivyo,kwa upande wake mgombea huyo mbali na kushukuru mapokezi ofisini hapo pia alihaidi kufuata maagizo ya chama hicho na kusisitiz kwamba atafuata maagizo ya kanuni hizo kwa umakini mkubwa.
Fute,alitangaza rasmi kuinga katika kinyang”anyiro hicho kupitia CCM huku akijitapa kwamba amejipima na kubaini anatosha kuwa mwakilishi wa jimbo la Arusha mjini kwa kuwa amegundua kuna ombwe la uongozi.


Mustafa Panju kuingia katika mbio za ubunge Arusha mjini

Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Bushbucks Safaris iliyopo jijini Arusha, Mustafa Panju akiongea na vyombo mbalimbali vya habari ofisini kwake akitangaza rasmi kuwania kiti cha ubunge jimbo la Arusha mjini kupitia tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM.
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Bushbucks Safaris iliyopo jijini Arusha, Mustafa Panju akiongea na vyombo mbalimbali vya habari ofisini kwake ,akitangaza rasmi kuwania kiti cha ubunge jimbo la Arusha mjini kupitia tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM kushoto ni mke wake.

Na Pamela M, Arusha
JIMBO la Arusha ni moja ya jimbo ambalo linaonekana kuwa  ni jimbo lenye siasa komavu, kutokana na hali hiyo limeonekana kuongoza kwa vurugu na uvunjifu wa amani , ambapo kupitia kwa Mtangaza nia wa ubunge jimbo la Arusha mjini  Mustafa Panju amewahakikishia wananchi kurudisha amani hiyo. Jimbo hilo ambalo linashikiliwa na Mbunge wa Arusha mjini kupitia Chadema ,Godbless Lema ambaye hivi sasa ametangaza tena kulitaka jimbo, ambapo hadi hivi sasa jumla ya wagombea 18 kupitia Chama cha Mapinduzi wamejitokeza kumg’oa mbunge huyo.Akizungumza na waandishi wa habari jana wakati akitangaza nia ya kuwania ubunge kupitia Chama cha Mapinduzi , Panju alisema kuwa ipo sababu ya kurudisha jimbo hilo mikononi mwa CCM kwa kuwa CCM ni chama kinachopenda amani na kinachodumisha amani.‘kila mmoja anatambua jinsi ambavyo jiji la Arusha hivi sasa halina amani kabisa na hakuna mtu anayedhubutu hata kutembea usiku , ila nitahakikisha linakuwa jiji la amani na utulivu na kuwawezesha wananchi wake kufanya shughuli zao bila hofu yoyote’alisema Panju. Alifafanua zaidi kuwa,mbali na kurejesha amani jijini Arusha atahakikisha anaondoa makundi mbalimbali yaliyopo miongoni mwa wananchi kwa kuwafanya wawe wamoja na wenye ushirikiano ili kuleta mabadiliko katika jimbo la Arusha kwa ujumla.
Pia alisema kuwa,wagombea wote wa nafasi ya ubunge katika chama ni wajibu wao kujenga Undugu,Upendo, na urafiki wakati wote ili kuepuka kujenga makundi ndani ya chama kwa misingi mbalimbali ya ukabila, udini na hata urangi. Panju alisema kuwa, swala la kuwepo kwa makundi na vikundi katika vyama na kwa wananchi linapaswa kuangaliwa kwa umakini kwani likiendelea kuwepo linajenga uhasama ndani ya chama  na pia uhasama unaoleta ubaguzi ndani ya nchi kwa ujumla .