TUTUMIE MAONI AU HABARI KUPITIA EMAIL: clickhabari@gmail.com AU SIMU: +255 7557 758 909, : CCM MBELE KWA MBELE 2015

MGOMBEA UBUNGE VITI MAALUMU ARUSHA,NEEMA AHAIDI KUINUA VIJANA KIUCHUMI

Katibu wa vijana umoja wa vijana  UVCCM wilaya ya Arusha mjini Jamali Khimji akimkabidhi fomu ya ubunge viti maalum Bi.Neema Kiusa(27)katika ofisi za umoja huo jijini Arusha, ahaidi kuinua vijana kiuchumi endapo atapata nafasi ya kuwa Mbunge wa vijana Mkoa wa Arusha.
Neema Kiusa(27) Mgombea ubunge viti maalumu kupitia  chama cha Mapinduzi ambaye pia ni mjumbe wa baraza la vijana wilaya ya Longido akionyesha fomu aliyochukua leo.
Neema Kiusa(27)Mgombea ubunge viti maalumu kupitia  chama cha Mapinduzi ambaye pia ni mjumbe wa baraza la vijana wilaya ya Longido akitoka katika ofisi za umoja wa vijana wa ccm mkoa wa Arusha(UVCCM)baada ya kuchukua fomu
Mgombea ubunge kupita kundi la vijana (UVCCM) Neema Kiusa  leo amechukua fomu ya kuwania nafasi ya ubunge viti maalumu Mkoa wa Arusha,ambapo amesema kuwa shauku yake kubwa ni kuwatumikia vijana kwa kutatua changamoto ya ajira
Neema ambaye pia ni mjumbe wa baraza la vijana Wilaya ya Longido alisema kuwa ndoto yake ya kuwatumikia vijana ni ndoto yake ya muda mrefu sana hivyo endapo atapata nafasi hiyo atashirikiana na vijana bega kwa bega kuleta maendeleo katika Mkoa wa Arushaa
Pia mgombea huyo alitoa shukrani kwa mume wake  anayempa ushirikiano mkubwa wa kufanikisha ndoto yake ya kutumikia vijana ambapo aliwataka wanaume wengine kuonyesha ushirikiano kwa wake zao endapo wataonyesha nia ya kuwania nafasi za uongozi
Kwa upande wake Katibu wa vijana UVCCM wilaya ya Arusha mjini Jamali Khimji amewataka vijana wa chama cha mapinduzi kujitokeza kwa wingi kuchukua fomu za nafasi za ubunge viti maalumu kundi la vijana katika mkoa wa Arusha
Khimji alisema kuwa kijana anayetakiwa kuchukua fomu ya kuwania nafasi hiyo ni kijana wa kwanzia umri wa miaka 21-30 na awe ametimiza vigezo vya chama hicho

CCM ARUSHA HAIJAPATA MGOMBEA

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Arusha, kimesema hakina mgombea ubunge wa Jimbo la Arusha Mjini, aliyeandaliwa hadi sasa.

Kimesema mgombea mwenye sifa za kulikomboa jimbo hilo, ambalo liko Chadema, hajajitokeza mpaka sasa. Akizungumza na mwandishi wa gazeti hili hivi karibuni, Katibu wa CCM wa Wilaya ya Arusha ,Feruzi Banno alisema chama kina utaratibu wake wa kampeni na chama hakina mgombea aliyeandaliwa kwa kuwa muda wa kuandaa wagombea bado haujatangazwa.


Banno alisema hayo alipotakiwa, kufafanua kauli zilizozagaa jijini Arusha kuwa chama hicho kimemwandaa mmoja wa wagombea (jina tunalo) ambaye yuko mstari wa mbele kulitaka jimbo hilo kwa udi na uvumba na tayari ameanza harakati za kampeni kwa kushirikiana na baadhi ya viongozi wa CCM kata, wilaya na mkoa.


Alisema taarifa hizo zimekuwa zikisambazwa na wana CCM wenye kutaka ubunge Jimbo la Arusha, ambao wanaoana kama wanatengwa. Alisema kura za maoni za kumsaka mgombea ubunge ndani ya chama, ndizo zitakazoamua na si vinginevyo na kamwe chama hakitambeba mwana CCM .


Pamoja na hayo yote, Katibu huyo alisema Jimbo la Arusha lenye asilimia kuwa ya vijana, linahita mgombea mwenye kujichanganya katika rika zote na anayekubalika bila ya kubabaisha,kwani huyo atafanya chama kufanya kazi kwa urahisi na sio ngumu katika kampeni.


Banno alisema kuwa CCM inahamu ya kulikomboa Jimbo la Arusha Mjini hivyo hatuhitaji mgombea mzigo, ambaye itafika siku ya mwisho tukaanza kulaumiana hilo halitakubalika kamwe kwa uongozi wa chama wilaya. ‘’Tunataka mgombea kijana, mwenye kujichanganya katika vijiwe mbalimbali vya Jiji la Arusha na mwenye kujulikana katika kila kona ya Jimbo la Arusha na mgombea huyo bado hajajitokeza hadharani.


Hiyo itasaidia chama kufanya kazi ndogo sana lakina hatutaki mgombea ambaye chama kitafanya kazi ya ziada kumnadi, hilo halitakubalika kamwe. ‘’ Baadhi ya wana CCM waliojitokeza na kuonesha nia ya kuwania ubunge Jimbo la Arusha Mjini ni Kamanda wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana (UVCCM) Mkoa wa Arusha , Philemon Mollel na Wakili wa Kujitegemea, Victor Njau.


Mwingine ni Mjumbe wa Baraza Kuu la Vijana Taifa, Dk Arod Adamson na Deo Mtui.

MGOMBEA URAIS KUPITIA CCM DR. JOHN POMBE MAGUFULI AWASILI JIJINI DAR ES SALAAM, AJITAMBULISHA KWA WANA DAR ES SALAAM

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dr. John Pombe Magufuli pamoja na Mgombea Mwenza Mama Samia Suluhu wakishuka kwenye ndege mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa Ndege wa Mwalimu J.K.Nyerere na kulakiwa na viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali Mkoa wa Dar es salaam, Ambapo baadae Wagombea hao walitambulishwa kwenye mkutano mkubwa wa Hadhara katika viwanja vya Zakhem Mbagala jijini Dar es salaam.
Inaendelea......

Dk Magufuli: Sitaogopa mtu yeyote

Mgombea Urais kupitia Chama cha CCM kwenye uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu, Dk John Magufuli akihutubia Mkutano wa hadhara katika viwanja vya Zakheim Mbagala, Dar es Salaam jana.
Inaendelea.................

Historia ya Samia Suluhu Hassan wa CCM

Chama tawala nchini Tanzania CCM ambayo imekuwa katika kongamano la kitaifa mjini Dodoma ilimchagua bibi huyo mwenye umri wa miaka 54 mchache wa maneno na mwenye asili ya Zanzibar kushirikiana na dokta Magufuli.
Lakini bi Samia Suluhu Hassanni Nani ?
Bi Samia Suluhu Hassan ni mtanzania mwenye asili ya Zanzibar
Kiongozi huyu pia amewahi kushikilia nyadhifa za uwaziri katika Serikali ya Muungano na ya Zanzibar akihudumu kama waziri katika afisi ya makamu wa rais
Inaendelea............

MFAHAMU MKE WA MGOMBEA JOHN POMBE MAGUFULI.


SOMA HAPA ALICHOANDIKA MTANDAONI LOWASA BAADA YA MAGUFULI KUTEULIWA , KAULI YAKE YAELEZWA KUWA NA UTATA


JK amfananisha Magufuli na 'tingatinga'

Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akiwa amewanyanyua mikono mgombea urais kupitia chama hicho, Dk John Magufuli na mgombea mwenza wake, Samia Suluhu Hassan mbele ya wajumbe wa Mkutano Mkuu wa chama hicho, mjini Dodoma jana. Picha na Edwin Mjwahuzi   

Magufuli kuipeperusha CCM, UKAWA na mgombea wake, BVR yasogezwa mbele Dar

Ni Jumatatu nyingine tena leo Julai 13 imekupita. 

Waziri wa Ujenzi Dk. John Magufuli ateuliwa kuwa mgombea Urais kupitia CCM na ameahidi kutokukiangusha Chama hicho, huku akimteua Samia Suluhu Hassan kama mgombea mwenza.

Ulinzi wa nyumbani kwa Dk. John Magufuli umeimarishwa baada ya kutangazwa kuwa Mgombea Urais kupitia chama cha CCM, Viongozi wa Vyama vya upinzani UKAWA wasema hawatishwi na John Magufuli na wamejipanga kumtangaza rasmi mgombea wao wa Urais kesho.

Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC imetangaza kusogezwa mbele kwa zoezi la uandikishaji wa kupiga kura kwa Dar es salaam kutoka Julai 16 hadi Juali 22.

JK amfananisha Magufuli na 'tingatinga'

Mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dk John Pombe Magufuli ameelezewa na watu mbalimbali kuwa ni mchapakazi, makini, asiyependa uvivu, lakini Rais Jakaya Kikwete amehitimisha yote kwa kumpachika jina la “tingatinga”

Urais CCM........Magufuli Apata Ushindi wa Kishindo


Chama  cha  mapinduzi, CCM kimemteua  Dr .Magufuli  kuwa  mgombea  wa  Urais  2015.

Uteuzi wa  Dr. Magufuli  umetokana na  ushindi  wa  kishindo  alioupata  baada  ya  mkutano  mkuu  kukutana jana   usiku  kwa  ajili  ya  kupiga  kura  ili  kupata  jina moja  kati  ya  matatu  yaliyokuwa  yamependekezwa  na  Halmashauri  kuu  ya  CCM.

 Matokeo  ni  kama  ifuatavyo
1.Magufuli.....87%
2. Amina.......10%
3.Migiro......3%