Arusha. Binti wa Waziri mkuu wa
zamani, Edward Sokoine, Namelock Sokoine ameshinda kura za maoni
kugombea ubunge Jimbo la Monduli kupitia CCM huku mkwe wa Lowassa, Siyoi
Sumari akishindwa Jimbo la Arumeru Mashariki.
Namelock
ambaye ni mbunge wa Viti Maalumu (CCM) alipata kura 29,582 akifuatiliwa
na Loota Sanare aliyepata kura 8,809 na nafasi ya tatu, ilichukuliwa na
Lolinyu Mkoosu aliyepata kura 235 na Payani Leyani akipata kura 226.
Arumeru Mashariki: Sumari
aliyewania jimbo hilo kwa mara ya kwanza baada kifo cha baba yake
Jeremia Sumari na kushindwa na Joshua Nassari wa Chadema alipata kura
kura 3,664 dhidi ya 12,071 za John Pallangyo. Mshindi wa tatu alikuwa ni
William Sarakikya ambaye alipata kura 3,552 na wagombea hao waliwaacha
mbali wapinzani wao wengine wanne.
Arusha Mjini:
Katika Jimbo la Arusha Mjini, mfanyabiashara Philemon Mollel ameshinda
kwa kura 5,320, akifuatiliwa na mfanyabiashara mwingine Justine Nyari
aliyepata kura 1,894 na nafasi ya tatu, ilichukuliwa na Moses Mwizarubi
aliyepata kura 1,205.
Karatu: Dk Willibrod Lorry alishinda baada ya kupata kura 17,711, Rajabu Malewa (911), John Dado (745) na Joshua Mwambo (67).
Masele ambwaga Mlingwa
Naibu
Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Steven Masele amembwaga
waziri mwingine wa zamani, Dk Charles Mlingwa baada ya kupata 70,900
dhidi ya 669 za mpinzani wake. Wagombea wengine Abdallah Seni alipata
kura 391, Erasto Kwilasa (232), Hassan Athuman (164), Mussa Ngangala
(116), Hatibu Malimi (69), Wille Mzava (65) na Tara Omari (43).
Ushetu: Elias Kwandikwa (11,554) Isaya Sino (5,241) na Elfaidi Sikuli (2,007).
Kahama Mjini: Jumanne
Kishimba (9,754), Kintoki Godwin (433), Nkuba Charles (389), Bundala
Maiko (284), Sazia Robert (257), Kapela Robert (135), Ngalawa Adamu
(126), Luhende Jerard (106), Malele Charles (91), Tunge John kura (78),
Mpangama Deogratias (57), Machunda Eliakimu (56), Masanja Andrew (48) na
Kambarage Masusu (28).
Msalala: Ezekiel
Maige (11,575), Emmanuel Kipole (1,197), John Sukili (962), Nicholas
Mabula (668), Maganza Mashala (597), John Lufunga (29) na Wankia Welema
(14).
Solwa: Mbali ya matokeo ya kata
moja ambayo imerudia uchaguzi, Ahamed Salum alikuwa akiongoza kwa kura
17,485 akifuatiwa na Amos Mshandete (2,028), Cyprian Mhoja (1,586),
Luhende Richard (1,273), Kasile Paul (637), Gabriel Shija (361), Renatus
Chokala (357) na Hosea Somi (255).
Kishapu:
Kabla ya matokeo ya kata tatu, Suleiman Nchambi alikuwa akiongoza kwa
kura 13,443, William Bonda (6,143), Kishiwa Kapale (500), Limbe Moris
(393), Heke Bulugu (356) na Timoth Ndanya (193).
Mawaziri watamba Kanda ya Ziwa
Waziri
wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dk Titus Kamani ameshinda kura za
maoni Jimbo la Busega baada ya kupata kura 10,697 dhidi ya mbunge wa
zamani wa jimbo hilo, Dk Rafael Chegeni aliyepata kura 9,661. Buchosa:
Naibu Waziri wa Uchukuzi, Dk Charles Tizeba ameibuka mshindi kwa kupata
kura 26,368 dhidi ya Eston Majaliwa aliyepata 9,213.
Misungwi:
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Kitwanga ameibuka mshindi
kwa kura 26,171, akimwangusha Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Jacob
Shibiliti aliyepata kura 7,009. Shomari Chalamila alipata kura 1,840, Dk
Makene Doshi (1,339), Cleophace Jerome (1,051).
Ilemela:
Mkuu wa Wilaya ya Iringa Angelina Mabula ameibuka mshindi katika Jimbo
la Ilemela
kwa kupata kura 6,324 mbele ya Barnabas Mathayo (3,562), John Buyamba (1,167) na wagombea wengine 16.
kwa kupata kura 6,324 mbele ya Barnabas Mathayo (3,562), John Buyamba (1,167) na wagombea wengine 16.
Tabora Kaskazini: Almasi Maige (9,466), Shaffin Sumari (6,392) na Joseph Kidawa (5,965).
Bariadi: Andrew Chenge (20,200), Masanja Kadogosa (2,986) na Cosmas Manula (270).
Meatu: Salum Mbuzi (13,180), Oscar Maduhu (2,988), Romano Thomas (358) na Donard Jinasa (350).
Itilima: Njallu Daudi (44,486), Simon Ngagani (2,759) na Danhi Makanga (814).