Stori kuhusu Siasa zinapewa nafasi kubwa sana sasa hivi, Tanzania inaingia kwenyeUchaguzi Mkuu Mwezi October 2015… Tayari wapo waliotangaza Kugombea nafasi mbalimbali lakini macho ya wengi yako kwenye nafasi ya Urais, mpaka sasa kuna majina zaidi ya 35 ya watu waliotangaza Kugombea nafasi ya Urais kupitia CCM.
Rais Kikwete yuko Dodoma, imenifikia hii Ripoti ya kilichoendelea jana wakati wa Kikao cha Kamati ya Usalama na Maadili cha CCM.
1. Kikao cha Kamati ya Usalama na Maadili-CCM kimeanza saa 8 mchana huu hapa Dodoma chini ya Mwenyekiti wake Ndugu@jmkikwete. #CCMInaamua
— CCM Youth League (@vijanaccm) July 8, 2015
2. Kikao kina wajumbe 13, wakiwemo M/kiti wa CCM, Makamu M/kiti na Katibu Mkuu, na kinajadili makada 38 waliochukua fomu za kugombea Urais.
— CCM Youth League (@vijanaccm) July 8, 2015
3. Kikao hiki ni cha juu kabisa katika Chama kinachojadili mwenendo, tabia, uadilifu, rekodi za utendaji na nidhamu ya kila mgombea.
— CCM Youth League (@vijanaccm) July 8, 2015
Taarifa Waziri Mkuu hatakuwa tena kiongozi wa Wabunge wa CCM, badala yake Wabunge watachagua kiongozi wao asiyekuwa na wadhifa wa Uwaziri.
— CCM Youth League (@vijanaccm) July 8, 2015
Hii ni Tweet ya Rais JK aliyoweka muda mfupi uliopita
Siasa za makundi ni siasa za maslahi. Siasa zinazolenga kutatua changamoto za Taifa hazina kundi bali humgusa kila mwenye nia njema na nchi.
— Jakaya Kikwete (@jmkikwete) July 9, 2015