Matokeo ya CCM Ubunge
Arusha. Binti wa Waziri mkuu wa
zamani, Edward Sokoine, Namelock Sokoine ameshinda kura za maoni
kugombea ubunge Jimbo la Monduli kupitia CCM huku mkwe wa Lowassa, Siyoi
Sumari akishindwa Jimbo la Arumeru Mashariki.
Namelock
ambaye ni mbunge wa Viti Maalumu (CCM) alipata kura 29,582 akifuatiliwa
na Loota Sanare aliyepata kura 8,809 na nafasi ya tatu, ilichukuliwa na
Lolinyu Mkoosu aliyepata kura 235 na Payani Leyani akipata kura 226.
Arumeru Mashariki: Sumari
aliyewania jimbo hilo kwa mara ya kwanza baada kifo cha baba yake
Jeremia Sumari na kushindwa na Joshua Nassari wa Chadema alipata kura
kura 3,664 dhidi ya 12,071 za John Pallangyo. Mshindi wa tatu alikuwa ni
William Sarakikya ambaye alipata kura 3,552 na wagombea hao waliwaacha
mbali wapinzani wao wengine wanne.
Arusha Mjini:
Katika Jimbo la Arusha Mjini, mfanyabiashara Philemon Mollel ameshinda
kwa kura 5,320, akifuatiliwa na mfanyabiashara mwingine Justine Nyari
aliyepata kura 1,894 na nafasi ya tatu, ilichukuliwa na Moses Mwizarubi
aliyepata kura 1,205.
Karatu: Dk Willibrod Lorry alishinda baada ya kupata kura 17,711, Rajabu Malewa (911), John Dado (745) na Joshua Mwambo (67).
Masele ambwaga Mlingwa
Naibu
Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Steven Masele amembwaga
waziri mwingine wa zamani, Dk Charles Mlingwa baada ya kupata 70,900
dhidi ya 669 za mpinzani wake. Wagombea wengine Abdallah Seni alipata
kura 391, Erasto Kwilasa (232), Hassan Athuman (164), Mussa Ngangala
(116), Hatibu Malimi (69), Wille Mzava (65) na Tara Omari (43).
Ushetu: Elias Kwandikwa (11,554) Isaya Sino (5,241) na Elfaidi Sikuli (2,007).
Kahama Mjini: Jumanne
Kishimba (9,754), Kintoki Godwin (433), Nkuba Charles (389), Bundala
Maiko (284), Sazia Robert (257), Kapela Robert (135), Ngalawa Adamu
(126), Luhende Jerard (106), Malele Charles (91), Tunge John kura (78),
Mpangama Deogratias (57), Machunda Eliakimu (56), Masanja Andrew (48) na
Kambarage Masusu (28).
Msalala: Ezekiel
Maige (11,575), Emmanuel Kipole (1,197), John Sukili (962), Nicholas
Mabula (668), Maganza Mashala (597), John Lufunga (29) na Wankia Welema
(14).
Solwa: Mbali ya matokeo ya kata
moja ambayo imerudia uchaguzi, Ahamed Salum alikuwa akiongoza kwa kura
17,485 akifuatiwa na Amos Mshandete (2,028), Cyprian Mhoja (1,586),
Luhende Richard (1,273), Kasile Paul (637), Gabriel Shija (361), Renatus
Chokala (357) na Hosea Somi (255).
Kishapu:
Kabla ya matokeo ya kata tatu, Suleiman Nchambi alikuwa akiongoza kwa
kura 13,443, William Bonda (6,143), Kishiwa Kapale (500), Limbe Moris
(393), Heke Bulugu (356) na Timoth Ndanya (193).
Mawaziri watamba Kanda ya Ziwa
Waziri
wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dk Titus Kamani ameshinda kura za
maoni Jimbo la Busega baada ya kupata kura 10,697 dhidi ya mbunge wa
zamani wa jimbo hilo, Dk Rafael Chegeni aliyepata kura 9,661. Buchosa:
Naibu Waziri wa Uchukuzi, Dk Charles Tizeba ameibuka mshindi kwa kupata
kura 26,368 dhidi ya Eston Majaliwa aliyepata 9,213.
Misungwi:
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Kitwanga ameibuka mshindi
kwa kura 26,171, akimwangusha Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Jacob
Shibiliti aliyepata kura 7,009. Shomari Chalamila alipata kura 1,840, Dk
Makene Doshi (1,339), Cleophace Jerome (1,051).
Ilemela:
Mkuu wa Wilaya ya Iringa Angelina Mabula ameibuka mshindi katika Jimbo
la Ilemela
kwa kupata kura 6,324 mbele ya Barnabas Mathayo (3,562), John Buyamba (1,167) na wagombea wengine 16.
kwa kupata kura 6,324 mbele ya Barnabas Mathayo (3,562), John Buyamba (1,167) na wagombea wengine 16.
Tabora Kaskazini: Almasi Maige (9,466), Shaffin Sumari (6,392) na Joseph Kidawa (5,965).
Bariadi: Andrew Chenge (20,200), Masanja Kadogosa (2,986) na Cosmas Manula (270).
Meatu: Salum Mbuzi (13,180), Oscar Maduhu (2,988), Romano Thomas (358) na Donard Jinasa (350).
Itilima: Njallu Daudi (44,486), Simon Ngagani (2,759) na Danhi Makanga (814).
Waliojitokeza Kuwania Ubunge Kwa Tiketi Ya CCM.
Arumeru Mashariki: Elirehema Kaaya, Jackson Ezekiel, John Sakaya. Angela Palangyo, William Sarakikya, Dk Daniel Pallangyo na Siyoi Sumari.
Longido:
Philip Kitesho, Dk Stivin Kiluswa, Lee Mamaseta, Daniel Marari, Lesioni
Mollel, Joseph Kulunju, Lemayani Logoliye na Emmanuel Sirikwa.
Monduli: Sakata Babuti, Loota Sanare, Loliayu Mkoosi, Namelock Sokoine, Mbayani Kayai na Amani Turongei.
Arumeru Magharibi: Loy Thomas Sabaya, Daudi Mollel, Elisa Mollel, Osilili Losai, Henri Majola, Lekoko Piniel na Lomoni Mollel.
Ngorongoro: Eliaman Laltaika, Elias Ngolisa, Joseph Parsambei, Patrick Kasongo, William Ole Nasha na Saning’o Telele.
Karatu: John Dodo, Dk Willbrod Rorri, Joshua Mbwambo na Rajabu Malewa.
Arusha Mjini:
Mustapha Panju, Justin Nyari, Philemon Mollel, Victa Njau, Thomas
Munisi, Hamis Migire, Admund Ngemera, Moses Mwizarubi, Ruben Mwikeni,
Endrew Lymo, Salehe Kiluvia, Lukiza Makubo, Mohammed Omar na Emmanuel
ole Ngoto.
Mkalama: Mgana Msindai,
Profesa Shaban Mbogho, Nakey Sule, Orgenes Joseph Mbasha na Allan Kiula,
Emmanuel Mkumbo, Dk Kissui Kissui, William Makali, Kyuza Kitundu, Dk
Charels Mgana, Salaome Mwambu, Francis Mtinga, Dk George Mkoma na Lameck
Itungi.
Manyoni Magharibi: John
Lwanji, Eliphas Lwanji, Jamal Kuwingwa, Jane Likuda, Mohammed Makwaya,
Yahaya Masare, Athumani Masasi, Yohana Msita, Moshi Mmanywa, Adimini
Msokwa, Dk Mwanga Mkayagwa, Rashidi Saidi na Francis Shaban.
Manyoni Mashariki: Dk Pius Chaya, Joseph Chitinka, Alex Manonga, Jumanne Mtemi, Daniel Mtuka, Harold Huzi na Gaitani Romwad.
Singida Mashariki: Jonathan Njau, Hamisi Maulid, Mdimi Hongoa, Jocab Kituu, Emmanuel Hume na Martin Lissu.
Ikungi Magharibi: Dinawi Gabaraiel, Hamisi Lissu, Wilson Khambaku, Dk Hamisi Mahuna, Dk Grace Puja, Yona Makala, Elibariki Kingu na Hamisi Ngila.
Iramba Magharibi: Mwigulu Nchemba, David Jairo, Juma Kilimba na Amon Gyuda.
Singida Mjini: Hassan Mazala, Amani Rai, Mussa Sima, Leah Samike, Philemon Kiemi na Juma Kidabu.
Singida Kaskazini: Lazaro Nyalandu, Amosi Makiya, Justin Monko, Michael Mpombo, Sabasaba Manase, Yahana Sinton, Mugwe na Aron Mgogho.
MTANGAZA NIA UBUNGE JIMBO LA ARUSHA MJINI, MOSSES MWIZARUBI AKICHUKUA FOMU
Ndugu zangu Wana-Arusha na Watanzania kwa ujumla, kwa heshima na
unyenyekevu mkubwa, napenda kuwajulisha kwamba jana nilichukua fomu za
kuomba kugombea Ubunge wa Jimbo la Arusha Mjini. Naomba mnikumbuke
katika sala zenu, hasa wale ambao ni wadau wa maendeleo ya Taifa letu.
Mungu ibariki Afrika, Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Arusha...
Katibu wa chama Cha Mapinduzi CCM Wilayani Arusha, Feruz Bano (Kulia) akimkabidhi fomu za kuwania kuteuliwa kuwa mgombea Ubunge katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika OKTOBA 25 mwaka huu.katika jimbo la Arusha mjini
Mgombea huyo alifika mbele ya ofisi za CCM wilayani hapa.Kuchukua fomu za kuwania kuteuliwa kuwa mgombea Ubunge katika Jimbo La Arusha Mjini. (kushoto) Ni Mwenyekiti wa Mtaa Wa Migungani, Bi Mary (katikati) Mkewe Agness Na (Kulia) Ndugu Mosses Mwizarubi
Mtangaza nia Ndugu Mosses Mwizarubi (Kushoto) akiongozana na Mkewe Agness(Katikati) NaKatibu wa chama Cha Mapinduzi CCM Wilayani Arusha, Feruz Bano(Kulia) Katika Picha ya Pamoja.

MGOMBEA UBUNGE VITI MAALUMU ARUSHA,NEEMA AHAIDI KUINUA VIJANA KIUCHUMI
Katibu wa vijana umoja wa vijana UVCCM wilaya ya Arusha mjini Jamali Khimji akimkabidhi fomu ya ubunge viti maalum Bi.Neema Kiusa(27)katika ofisi za umoja huo jijini Arusha, ahaidi kuinua vijana kiuchumi endapo atapata nafasi ya kuwa Mbunge wa vijana Mkoa wa Arusha.
Neema Kiusa(27) Mgombea ubunge viti maalumu kupitia chama cha Mapinduzi ambaye pia ni mjumbe wa baraza la vijana wilaya ya Longido akionyesha fomu aliyochukua leo.
Neema Kiusa(27) Mgombea ubunge viti maalumu kupitia chama cha Mapinduzi ambaye pia ni mjumbe wa baraza la vijana wilaya ya Longido akionyesha fomu aliyochukua leo.
Neema Kiusa(27)Mgombea ubunge viti maalumu kupitia chama cha Mapinduzi ambaye pia ni mjumbe wa baraza la vijana wilaya ya Longido akitoka katika ofisi za umoja wa vijana wa ccm mkoa wa Arusha(UVCCM)baada ya kuchukua fomu
Mgombea ubunge kupita kundi la vijana (UVCCM) Neema Kiusa leo amechukua fomu ya kuwania nafasi ya ubunge viti maalumu Mkoa wa Arusha,ambapo amesema kuwa shauku yake kubwa ni kuwatumikia vijana kwa kutatua changamoto ya ajira
Neema ambaye pia ni mjumbe wa baraza la vijana Wilaya ya Longido alisema kuwa ndoto yake ya kuwatumikia vijana ni ndoto yake ya muda mrefu sana hivyo endapo atapata nafasi hiyo atashirikiana na vijana bega kwa bega kuleta maendeleo katika Mkoa wa Arushaa
Pia mgombea huyo alitoa shukrani kwa mume wake anayempa ushirikiano mkubwa wa kufanikisha ndoto yake ya kutumikia vijana ambapo aliwataka wanaume wengine kuonyesha ushirikiano kwa wake zao endapo wataonyesha nia ya kuwania nafasi za uongozi
Kwa upande wake Katibu wa vijana UVCCM wilaya ya Arusha mjini Jamali Khimji amewataka vijana wa chama cha mapinduzi kujitokeza kwa wingi kuchukua fomu za nafasi za ubunge viti maalumu kundi la vijana katika mkoa wa Arusha
Khimji alisema kuwa kijana anayetakiwa kuchukua fomu ya kuwania nafasi hiyo ni kijana wa kwanzia umri wa miaka 21-30 na awe ametimiza vigezo vya chama hicho
CCM ARUSHA HAIJAPATA MGOMBEA
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Arusha, kimesema hakina mgombea ubunge wa Jimbo la Arusha Mjini, aliyeandaliwa hadi sasa.
Kimesema mgombea mwenye sifa za kulikomboa jimbo hilo, ambalo liko Chadema, hajajitokeza mpaka sasa. Akizungumza na mwandishi wa gazeti hili hivi karibuni, Katibu wa CCM wa Wilaya ya Arusha ,Feruzi Banno alisema chama kina utaratibu wake wa kampeni na chama hakina mgombea aliyeandaliwa kwa kuwa muda wa kuandaa wagombea bado haujatangazwa.
Banno alisema hayo alipotakiwa, kufafanua kauli zilizozagaa jijini Arusha kuwa chama hicho kimemwandaa mmoja wa wagombea (jina tunalo) ambaye yuko mstari wa mbele kulitaka jimbo hilo kwa udi na uvumba na tayari ameanza harakati za kampeni kwa kushirikiana na baadhi ya viongozi wa CCM kata, wilaya na mkoa.
Alisema taarifa hizo zimekuwa zikisambazwa na wana CCM wenye kutaka ubunge Jimbo la Arusha, ambao wanaoana kama wanatengwa. Alisema kura za maoni za kumsaka mgombea ubunge ndani ya chama, ndizo zitakazoamua na si vinginevyo na kamwe chama hakitambeba mwana CCM .
Pamoja na hayo yote, Katibu huyo alisema Jimbo la Arusha lenye asilimia kuwa ya vijana, linahita mgombea mwenye kujichanganya katika rika zote na anayekubalika bila ya kubabaisha,kwani huyo atafanya chama kufanya kazi kwa urahisi na sio ngumu katika kampeni.
Banno alisema kuwa CCM inahamu ya kulikomboa Jimbo la Arusha Mjini hivyo hatuhitaji mgombea mzigo, ambaye itafika siku ya mwisho tukaanza kulaumiana hilo halitakubalika kamwe kwa uongozi wa chama wilaya. ‘’Tunataka mgombea kijana, mwenye kujichanganya katika vijiwe mbalimbali vya Jiji la Arusha na mwenye kujulikana katika kila kona ya Jimbo la Arusha na mgombea huyo bado hajajitokeza hadharani.
Hiyo itasaidia chama kufanya kazi ndogo sana lakina hatutaki mgombea ambaye chama kitafanya kazi ya ziada kumnadi, hilo halitakubalika kamwe. ‘’ Baadhi ya wana CCM waliojitokeza na kuonesha nia ya kuwania ubunge Jimbo la Arusha Mjini ni Kamanda wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana (UVCCM) Mkoa wa Arusha , Philemon Mollel na Wakili wa Kujitegemea, Victor Njau.
Mwingine ni Mjumbe wa Baraza Kuu la Vijana Taifa, Dk Arod Adamson na Deo Mtui.

MGOMBEA URAIS KUPITIA CCM DR. JOHN POMBE MAGUFULI AWASILI JIJINI DAR ES SALAAM, AJITAMBULISHA KWA WANA DAR ES SALAAM
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dr. John Pombe Magufuli pamoja na Mgombea Mwenza Mama Samia Suluhu wakishuka kwenye ndege mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa Ndege wa Mwalimu J.K.Nyerere na kulakiwa na viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali Mkoa wa Dar es salaam, Ambapo baadae Wagombea hao walitambulishwa kwenye mkutano mkubwa wa Hadhara katika viwanja vya Zakhem Mbagala jijini Dar es salaam.
Inaendelea......
Dk Magufuli: Sitaogopa mtu yeyote
Mgombea Urais kupitia Chama cha CCM kwenye uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu, Dk John Magufuli akihutubia Mkutano wa hadhara katika viwanja vya Zakheim Mbagala, Dar es Salaam jana.
Inaendelea.................
Inaendelea.................
Historia ya Samia Suluhu Hassan wa CCM
Chama tawala nchini Tanzania CCM ambayo imekuwa katika kongamano la kitaifa mjini Dodoma ilimchagua bibi huyo mwenye umri wa miaka 54 mchache wa maneno na mwenye asili ya Zanzibar kushirikiana na dokta Magufuli.
Lakini bi Samia Suluhu Hassanni Nani ?
Bi Samia Suluhu Hassan ni mtanzania mwenye asili ya Zanzibar
Kiongozi huyu pia amewahi kushikilia nyadhifa za uwaziri katika Serikali ya Muungano na ya Zanzibar akihudumu kama waziri katika afisi ya makamu wa rais
Inaendelea............
Magufuli kuipeperusha CCM, UKAWA na mgombea wake, BVR yasogezwa mbele Dar
Ni Jumatatu nyingine tena leo Julai 13 imekupita.
Waziri wa Ujenzi Dk. John Magufuli ateuliwa kuwa mgombea Urais kupitia CCM na ameahidi kutokukiangusha Chama hicho, huku akimteua Samia Suluhu Hassan kama mgombea mwenza.
Ulinzi wa nyumbani kwa Dk. John Magufuli umeimarishwa baada ya kutangazwa kuwa Mgombea Urais kupitia chama cha CCM, Viongozi wa Vyama vya upinzani UKAWA wasema hawatishwi na John Magufuli na wamejipanga kumtangaza rasmi mgombea wao wa Urais kesho.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC imetangaza kusogezwa mbele kwa zoezi la uandikishaji wa kupiga kura kwa Dar es salaam kutoka Julai 16 hadi Juali 22.
JK amfananisha Magufuli na 'tingatinga'
Mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dk John Pombe Magufuli ameelezewa na
watu mbalimbali kuwa ni mchapakazi, makini, asiyependa uvivu, lakini
Rais Jakaya Kikwete amehitimisha yote kwa kumpachika jina la
“tingatinga”
Urais CCM........Magufuli Apata Ushindi wa Kishindo
Chama cha mapinduzi, CCM kimemteua Dr .Magufuli kuwa mgombea wa Urais 2015.
Uteuzi
wa Dr. Magufuli umetokana na ushindi wa kishindo alioupata
baada ya mkutano mkuu kukutana jana usiku kwa ajili ya kupiga
kura ili kupata jina moja kati ya matatu yaliyokuwa
yamependekezwa na Halmashauri kuu ya CCM.
Matokeo ni kama ifuatavyo
1.Magufuli.....87%
2. Amina.......10%
3.Migiro......3%
Magufuli alivyopiga chenga panga la CCM
Dar es Salaam. Kama alivyowashangaza wengi pale alipojitokeza
kuchukua fomu za kuomba kuteuliwa na CCM kuwania urais Mei 29 mwaka huu,
ndivyo Dk John Magufuli alivyowashangaza tena jana kufikia hatua hii ya
tano bora.
Bila makeke, majivuno wala majigambo, Magufuli
ambaye ni waziri wa ujenzi alipochukua fomu alisema tu kuwa kipaumbelea
chake ni kutekeleza ilani ya uchagzi ya CCM.
Hata katika safari yake ya kusaka wadhamini
mikoani, mbunge huyo wa Chato alikwenda kimya kimya, bila mbwembwe,
ahadi wala kukusanya mashabiki.
Bila shaka hiyo ndiyo siri yake ya ushindi, alihofia kukatwa mapema kwa kukiuka masharti ya chama, kama ilivyowatokea wengine.
Hata kabla hajachukua fomu, Dk Magufuli hakuwahi
kutangaza nia yake ya kuwania urais, hadi alipoibuka ghafla na papo hapo
akapenya hadi hatua hii muhimu, hadi alipolidokeza gazeti hili mjini
Dodoma.
Subscribe to:
Posts (Atom)